KUJINASIBISHA NA KUJIITA SALAFI

Published on by شبكة منهاج السنة النبوية ال

Hakika shukurani nyingi ni za Allah ndio kwake tunategemea na  kwake tunamuomba msamaha. Na tunajikinga kwa Allah kutokana na shari za nafsi zetu na uovu wa matendo yetu. Basi yule ambae Allah amemuongoza ndio ameongoka na yule ambae amempoteza hakuna atakae muongoa kamwe. Nashuhudia ya kwamba hakuna  mola apasae kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah pekeyake tu, na  wala hana mshirika katika Uungu wake. Na nashuhudia  Muhammad ndio Mtume wake.
{Enyi mlioamini. Mcheni Allah kama ipasavyo kumcha wala msife isipokuwa mmekwishakuwa waislaam kamili} Qur-an 3:102.
{Enyi watu mcheni molawenu ambae amekuumbeni ktk nafsi moja. Na akamuumba mkewe ktk nafsi ileile. Na akaeneza wanaume wengi na wanawake kutoka ktk wawili hao, na mcheni Allah ambae kwake mnamuomba na muwatazame jamaa hakika Allah ni mlinzi juu yenu.} [Qur-an 4:1]

{Enyi mlioamini muogopeni Allah na semeni maneno ya kweli. Atakutengenezeeni vizuri vitendo vyenu na atakusameheni madhambi yenu. Na anaemtii Allah na mtume wake, bilashaka amefanikiwa mafanikio makubwa} Qur-an 33:70-71.

Ama baada, Elewa ndugu Muislaam,-Allah akuwafikishe- hakika wafuwasi wa kweli wa Sunna za Mtumeni: Masalaf Assaleh (Wajawema waliotutangulia) mwenendo wa Wajawema waliotutangulia ni wajibu kwa kila Muislamu kuufuata kwa ushahidi wa Kitabu na Sunna, zimekuja dalili nyingi ndani yake, tukianza na dalili ya kwanza:

A) Kauli ya Mtume (Salallahu alehi wasallam): ((Watu bora ni wale ambao ni katika karne yangu mimi, kisha wanaofuata, kisha wanaofuata)) Muttafaqun aleihi.

B) Kasema tena Mtume (Salallahu alehi wasallam): ((Nautafarikiana Umma huu juu ya makundi Sabini na Tatu yote yataingia Motoni kasoro Moja tu (Kundi) ambalo niponalo mimi na Masahaba wangu)).

Utakuta katika Hadithi Mbili hizi tulizo zitoa zinaonyesha wazi mwenendo wa Masalafi unatafautiana kabisa na makundi (mikusanyiko) mingi yaliyopo katika Uislamu.

Dini kwetu sisi Masalafi ni kushikamana barabara na Kitabu na Sunna za Mtume (Salallahu alehi wasallam), na njia ya ufahamu na uelewa wa Dini hii ya Kislamu kwetu sisi Masalafi kama walivyo fahamu na kuelewa Salafussaleh (Wajawema aliotutangulia kabla yetu).

Kwa kuwa hakusema Mtume (Salallahu alehi wasallam) kundi ambalo nikonalo mimi (tu), bali aliendelea kusema: na Masahaba wangu, na maelezo haya yanaushahidi ndani ya Qur-ani, pale alipo sema Allah: {Na atakaemuasi Mtume, baada ya kubainikiwa uongofu na kafuata njia isiokuwa ya Waumini (Masahaba) tutamgeuza huko aliko geukia mwenyewe na tutamwingiza katika Jahannam, napo ni pahali pabaya kabisa pa Mtu kurudia} Qur-ani 4:115.

Na kasema tena Allah: {Na wale waliotangulia wakawa wakwanza katika Uislamu Muhajirina na Ansar, na wale waliowafuata kwa wema Allah amewaridhia nao wamemridhia, na amewaandalia mabustani yapitayo Mito chini yake, wakakae humo milele. Huku ndiko kufuzu kukumbwa} Qur-ani 9: 100.

Kasema Ibn Masoud Radhiyallahu anhu: ((Yoyote miongoni mwenu anaetakakuiga mwenendo, basi aige mwenendo wa wale waliokwisha fariki kwa sababu alie hai haminiki kupata fitna, hao ni Masahaba wa Mtume (Salallahu alehi wasallam), walikuwa ni watu bora katika Umma huu, na wenye nyoyo njema, nyoyo zilizo zama katika elimu, walikuwa sio watu wenyekujikalifisha, ni watu aliowachagua Allah kuwa ni marafiki wa Mtume wake na kusimamisha Dini yake, basi muzifahamu fadhila zao, na fuateni nyayo zao, na mshikamane mtakacho weza katika tabia na Dini yao,  kwa hakika walikuwa katika uongofu ulionyooka)). Tazama katika Kitabu “Jamie” J2 Uk 97.

Tambueni Enyi waja wa Allah: Yale yote waliyo kuwa nayo Masahaba wa Mtume (Salallahu alehi wasallam) katika kufahamu Dini ni uongofu mtupu, basi igeni mwenendo wao, na muyafanyie kazi waliyokuwanayo ndipo mtakapo ongoka.

Jambo lolote ambalo halikuwa katika zama za Masahaba Dini basi kamwe halitakuwa Dini leo hii, kasema Imam Malik -Allah amrehemu-: ((Hauta kuwa mwema mwisho wa Umma huu mpaka wafuate ule wema wawale wa mwanzo katika Umma huu)).

Kasema Ibn Masoud Radhiyallahu anhu: ((Fuateni wala msizue kwa hakika mmeshatoshelezwa)). Na kasema tena: ((Kwa hakika Sisi tunaiga wala hatuanzishi, na tunafuata wala hatuzui, hatutapotea endapo tutakapo shikamana na athari (za Masahaba))) Al Alkai.

Kasema tena Ibn Maoud Radhiyallahu anhu: ((Asiige mmoja wenu Dini yake kwa Mtu yoyote Yule, atakapo amini na yeye anaamini, na atakapo kufuru na yeye anakufuru, ikiwa hakuna budi kuiga basi waigeni walikwisha fariki, kwa sababu alie hai haiaminiki juu yake fitna)) tazama katika kitabu “Alhulya” J 1 Uk 136.

Kasema Hudhaifa Radhiyallahu anhu: ((Mcheni Allah Enyi kundi la wasomi, chukueni njia ya walio kabla yenu, Wallahi mtakapo wahi basi mmewahi (ushindi) wa mbali kabisa, na mtakapo wacha mkaenda kombo kulia na kushoto, mtapotea upotevu uliombali kabisa)). Katika masimulizi mengine imekuja: ((Fuateni njia yetu kwa hakika mtakapo fuata njia yetu mmeshinda ushindi ulio wa mbali kabisa)).

Masalafi ni: Masahaba na Matabiina na walio kuja baada yao hawa na wakawafuata kwa wema mpaka siku ya Kiama.

Kasema Imam Ahmad –Allah amrehemu-: ((Misingi ya Sunna kwetu sisi ni kushikamana na yale yote walio kuwa nayo Masahaba wa Mtume (Salallahu alehi wasallam) na kuiga mwenendo wao)).

Na  wafuasi wa Masahaba ni: Wale ambao walio shikamana na Kitabu na Sunna za Mtume (Salallahu alehi wasallam), na kushikamana na yote yale waliokubaliyana wale waliotangulia wakawa wa kwanza katika Uislamu miongoni mwa Muhajirina na Mansari.

Ewe Muislamu ndugu yangu namuomba Allah –akufufue pamoja na Masahaba-: Elewa kuwa Ahlusunna ndio Ahlu Alhadith ndio watu wa karibu kabisa  kwa Mtume (Salallahu alehi wasallam) ndio wao Ahlusunna waljamaa na ndio hawa hawa wenye kuwalingania watu katika Manhaji na dawa ya Salafi, na ndio hawa hawa kikundi ambacha kakielezea Mtume (Salallahu alehi wasallam) kwa kauli yake pale alipo sema: ((Kitabakia kikundi katika Umma wangu kipo juu ya haki kinadhihirika, hawatadhurika na watakae wafanyia khiyana wala wale watakae wakhalifu mpaka itakapo fika amri ya Allah)). Sahii mutawater.

Wamishawahi kujinasibisha na Masalafi au Usalafi pamoja na mwenendo wao Maimamu wakubwa kabisa na Wana wazuoni pamoja na Waislamu wengi kabla yetu na walio wafuata baada yao.

Miongoni mwao ni: Imam Ahmad, Al Bukhari, Al Auzai, Ashafi’e, Malik, Abu Hanifa , Sufiyan wote wawili,         Al Barbahari, Addaruqatni, Adhahabi, Ibn Alqayyim, na wale wote walio kuwa katika zama zao pamoja na wale waliokuja baada ya hawa ikaendelea mpaka zama zetu hizi –Allah awarehemu- wote.

Waliojiita kwa jina hili la Salafi si mmoja tu katika Wanawachuoni wakubwa wa Ahlusunna, bali waliojinasibisha na mwenendo wa Masalafi kundi kubwa kabisa la Wanawachuoni, kwa sababu na saba hii ya kujinasibiasha na Salafi ni na saba tukufu kabisa na iliotakasika ilio na ukarimu, kwa sababu kujinasibisha huko kunapendeza sana, na kujitambulisha kuwa wewe unajinasibisha na mwenendo wa wale wema walio kuwepo katika karne za kheri zilizo tangulia na watu walio bora kabisa baada ya Mitume ya Allah Subhana wataala  nao ni Masahaba wa Mtume wetu (Salallahu alehi wasallam).

Kasema Ibn Al Mundhir: ((Wassalaf, Wassalifu, Wassalfat, maana yake ni: Mkusanyiko wa wale waliotangulia)). Tazama kitabu “Lisan Al Arab” J 6 Uk 330..

Vile vile wameelezea Wanawachuoni wakubwa wa nasaba akiwemo Abdulkarim Assamani kasema: ((Assalafi  nasaba hii ni ya wale waliotutangulia na yoyote Yule atakaefuata mwenendo wao)). Tazama katika kitabu “Al Ansab” J 1 Uk 104.

Kasema Imam Adhahabi: ((Assalafi ni: Yoyote Yule atakae kuwa katika madhehebu ya Kisalafi)). Tazama kitabu “Assiyar” J 6 Uk 21.

Vile vile kasema Sheikh Al Isalam Ibn Taymiyya: ((Wala sio aibu kwa Yule atakae dhihirisha mwenendo wa Masalafi, na akajinasibisha nao, na akajitukuza nao, bali ni wajibu (kwa kila Mtu) kuyakubali hayo kwa sababu madhehebu ya Masalafi si vingine isipokuwa ni haki tu)). Tazama kitabu “Al Fatawa” J 4 Uk 149.

Kasema Imam Asafarini wakati akibainisha maana ya kisheria juu ya madhehemu ya Kisalafi: ((Muradi wa Madhehebu ya Kisalafi: Ni yale yote waliokuwa nayo Masahaba walio kirimiwa –Radhi za Allah ziwe juu yao- na miongoni mwa matabiin walio wafuata kwa wema, na wafuasi wao, na wana wazuoni wa Dini walioshuhudiwa kwa Uimamu wao, na sifa zao zilijulikana kwa kushikamana na Dini, na wakapokea Waislamu mafundisho yao waliokuja baada yao kwa waliowatangulia kabla yao, bila ya kujulikana Mtu huyu kwa Bida’a, au kutambulika kwa jina lisilo ridhiwa na Uislamu, kama Makhawarij, Rafidhia (Mashia), Maqadariya, …… na mfano yahawa)). Tazama kitabu “Lawami’e Al Anwar” J 2 Uk 126.

Imeshabainika kwa hakika mwenye kuitaka haki wajibu wa sheria kujinasibisha na Masalafi Wajawema waliotutangulia kwa na saba hii ya: ((Salaf au Assalafia) Asizani Mtu kujiita huku kuna pingana na sheria ya Allah ya kuitwa Waislamu pale alipo sema: {Yeye ndie alie kuiteni Waislamu} Qur-ani 22:78.

Kujiita Muislamu na kujiita Salafi kama tulivyo elezea hapo awali nasaba zote mbili hizi ni sahihi kabisa, nasaba ya kwanza (Uislamu) inatambulisha kuwa ni Dini, na nasaba ya Pili (Salafi au Salafia) inatambulisha kuwa ni njia au mwenendo wenye kuubainisha huu Uislamu ambao tunao uamini na kuitakidi.

Salafi yoyote Yeye anatangaza kuwa anaamini Uislamu ambao aliokuwa nao Mtume wetu (Salallahu alehi wasallam) na Masahaba wake wakarimu Radhiyallahu anhum kama alivyo sema: ((Kundi litakalo okoka ni lile ambalo ninalo mimi na Masahaba wangu)), na katika Hadithi nyengine kasema: ((Shikamaneni na Sunna zangu na Sunna za Makhalifa waongofu baada yangu)).

Kwa ujumla Dawa ya Salafi Inahimiza na kusisitiza kila wakati Waislamu wote juu ya wajibu kwao kufahamu Kitabu na Sunna kama walivyo fahamu wajawema aliotutangulia (Masalafi), ili kupata kumuakoa Muislamu huyu asije akapinda na kutoka katika njia iliyo nyooka na kupotea, Kila Salafi ni Mislamu bila shaka, lakini si kila Muislamu ni Salafi, inawezekana sana akawa Mtu Muislamu lakini Rafidhiya (Shia), au Ash’ariya, au Kharijiya. au Sufiyya, au Tablighiyya, au Ikhwaniyya, au Jama’at Ansar Sunna, au Tahririya, au Ibadhiyya, au   Qutt biyya, au Tahririya au Kadyaniyya ………. NK

Wabillahi Taufiq:

Abu Muadh Al Asbahi Assalafi

Masjid Sheikh Al Albani Dar es salaam

To be informed of the latest articles, subscribe:
Comment on this post
A
Jazaakallahu khyr
Mtume mwenyewe kajiita salaf
منهج الأنبياء:
NINI MAANA YA SALAF

➡️ Neno سلفي (salaf) linakusudiwa Wema waliopita na Al muhimu ni Wanafunzi na wafuasi wake mtume صل الله عليه وسلم yaani SALAFI ni MASAHABA

➡️ Mtu wa kwanza kutumia neno SALAFI ni mtume صل الله عليه وسلم
alipomwambia mwanae bi Faatima رضي الله عنها

"فاتقي الله واصبري فاءنه نعم السلف انا لك"

"Mche Allah na kuwa na Subra kwani mi ni Bora katika Salafi kwako"

Sahih Bukhaary - Mjeredi wa 8 hadith ya 58885 ????
Neno salafi limetumiwa sana na WANACHUONI kuanzia wa Kale mpaka baadhi wa zama za leo

Mfano IMAM AHMAD Ibn HAMBAL رحمه الله

IMAM ABU HANIFAH na wengi katika wao.

➡️ Salafiyyah (wanaofuata Mafundisho ya mtume kama walivyofahamu masahaba zake) Huitwa pia AHLU HADITH, AL ATHARI, AHLU SUNNAH WAL JAMAA na mfano wake

DAAWA YA SALAFI IMESIMAMIA MISINGI GANI?

➡️ Kufuata Aqeedah (ITIKADI) mambo yaliyofungamana na imaan kama Alivyofundisha mtume na ufahamu wa masahaba

➡️ Kushikamana na Sunnah vilivyo katika kila Ibaada na kujitenga na Bid'a kbs

➡️ Salafiyyah ni watu wanahimiza sana TAWHIID na kukaa mbali kbs na Shirk kwa nguvu zote

➡️ Salafiyyah huwaigiza Mtume na masahaba zake tabia zao njema walizoshikana nazo

➡️ Manhaj (njia yao Mtume na masahaba)

kwanini mtu afuate Manhaj SALAFI ni kwa sababu zifiatazo

DALILI katika QUR'AN

Allah Jalla wa'ala amesema

فَجَعَلْنَاهُمْ سَلَفًا وَمَثَلًا لِلْآخِرِينَ

Kisha tukawafanya kuwa watangulizi na mfano kwa wa baadaye...

Az Zukhruf : 56 ????

فَإِنْ آمَنُوا بِمِثْلِ مَا آمَنْتُمْ بِهِ فَقَدِ اهْتَدَوْا ۖ وَإِنْ تَوَلَّوْا فَإِنَّمَا هُمْ فِي شِقَاقٍ ۖ فَسَيَكْفِيكَهُمُ اللَّهُ ۚ وَهُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ

Basi wakiamini kama mnavyo amini nyinyi (Kundi la Masahaba na mtume), itakuwa kweli wameongoka. Na wakikengeuka basi wao wamo katika upinzani tu. Na Mwenyezi Mungu atakutosheni kukukingeni na shari yao, na Yeye ndiye Msikizi, Mjuzi....

Al Baqarah : 137 ????

KWANINI UFUATE MASAHABA (SALAFI) ufahamu wao kwa kila JAMBO?

dalili katika sunnah

Amesema mtume صل الله عليه وسلم

"خير الناس قرني، ثم الزين يلونهم، ثم الزين يلونهم"

"Watu bora kabisa ni Karne yangu (masahaba) kisha wataofuata (tabiin) kisha karne itakayofuata (at'bau Tabiin)

Imepokewa na Bukhaary????

Amesema Mtume صل الله عليه وسلم

"وانه من يعش منكم فسير ي اختلافا كثيرا

Yeyote atakayeishi muda mrefu baada yangu ataona Makasoro mengi katika dini hii

فعليكم بسنتي وسنة الخلفاء الراشدين المهديين

""Shikamaneni na sunnah zangu na Sunnah za Makhalifa wangu waongofu"

Ameipokea Abu Dawuud na At tirmidhy ????
Reply
A
Kwa bahati nzuri hakuna uthibitisho unasema jiiteni salafi Bali fuateni mienendo ya waja wema walio tanguliza .
Kua muislamu Bora ni Imani sahihi na matendo sahihi sio kujiiita Jina fulani
Wapo walio Bora kuliko sahaba ambao ni. Mitume Sasa mtu alisema nafata dini kama walivyielewa mituma bila matendo ni Bure

Makafiri wanataka dini yetu iwe kama ukristo Ukristo sio dini ya nabii Issa ni dini ilio fanyiwa marekebisho Bahati mbaya hakuna sheikh yoyote aliowaamrisha watu wajiite Jina fulani ili wawe waislamu Bora Bali waliwaamrisha wafanye matendo Bora ili wawe waislamu Bora taqwa Ndio itakua ubora katika uislam sio Jina fulani

Bahati mbaya. Ulamaa wa akhir zama wanauza vitu katika dini. Jina Bora ni Islam kwa mujibu wa Quran na hadith
Reply
A
منهج الأنبياء:
NINI MAANA YA SALAF

➡️ Neno سلفي (salaf) linakusudiwa Wema waliopita na Al muhimu ni Wanafunzi na wafuasi wake mtume صل الله عليه وسلم yaani SALAFI ni MASAHABA

➡️ Mtu wa kwanza kutumia neno SALAFI ni mtume صل الله عليه وسلم
alipomwambia mwanae bi Faatima رضي الله عنها

"فاتقي الله واصبري فاءنه نعم السلف انا لك"

"Mche Allah na kuwa na Subra kwani mi ni Bora katika Salafi kwako"

Sahih Bukhaary - Mjeredi wa 8 hadith ya 58885 ????
Neno salafi limetumiwa sana na WANACHUONI kuanzia wa Kale mpaka baadhi wa zama za leo

Mfano IMAM AHMAD Ibn HAMBAL رحمه الله

IMAM ABU HANIFAH na wengi katika wao.

➡️ Salafiyyah (wanaofuata Mafundisho ya mtume kama walivyofahamu masahaba zake) Huitwa pia AHLU HADITH, AL ATHARI, AHLU SUNNAH WAL JAMAA na mfano wake

DAAWA YA SALAFI IMESIMAMIA MISINGI GANI?

➡️ Kufuata Aqeedah (ITIKADI) mambo yaliyofungamana na imaan kama Alivyofundisha mtume na ufahamu wa masahaba

➡️ Kushikamana na Sunnah vilivyo katika kila Ibaada na kujitenga na Bid'a kbs

➡️ Salafiyyah ni watu wanahimiza sana TAWHIID na kukaa mbali kbs na Shirk kwa nguvu zote

➡️ Salafiyyah huwaigiza Mtume na masahaba zake tabia zao njema walizoshikana nazo

➡️ Manhaj (njia yao Mtume na masahaba)

kwanini mtu afuate Manhaj SALAFI ni kwa sababu zifiatazo

DALILI katika QUR'AN

Allah Jalla wa'ala amesema

فَجَعَلْنَاهُمْ سَلَفًا وَمَثَلًا لِلْآخِرِينَ

Kisha tukawafanya kuwa watangulizi na mfano kwa wa baadaye...

Az Zukhruf : 56 ????

فَإِنْ آمَنُوا بِمِثْلِ مَا آمَنْتُمْ بِهِ فَقَدِ اهْتَدَوْا ۖ وَإِنْ تَوَلَّوْا فَإِنَّمَا هُمْ فِي شِقَاقٍ ۖ فَسَيَكْفِيكَهُمُ اللَّهُ ۚ وَهُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ

Basi wakiamini kama mnavyo amini nyinyi (Kundi la Masahaba na mtume), itakuwa kweli wameongoka. Na wakikengeuka basi wao wamo katika upinzani tu. Na Mwenyezi Mungu atakutosheni kukukingeni na shari yao, na Yeye ndiye Msikizi, Mjuzi....

Al Baqarah : 137 ????

KWANINI UFUATE MASAHABA (SALAFI) ufahamu wao kwa kila JAMBO?

dalili katika sunnah

Amesema mtume صل الله عليه وسلم

"خير الناس قرني، ثم الزين يلونهم، ثم الزين يلونهم"

"Watu bora kabisa ni Karne yangu (masahaba) kisha wataofuata (tabiin) kisha karne itakayofuata (at'bau Tabiin)

Imepokewa na Bukhaary????

Amesema Mtume صل الله عليه وسلم

"وانه من يعش منكم فسير ي اختلافا كثيرا

Yeyote atakayeishi muda mrefu baada yangu ataona Makasoro mengi katika dini hii

فعليكم بسنتي وسنة الخلفاء الراشدين المهديين

""Shikamaneni na sunnah zangu na Sunnah za Makhalifa wangu waongofu"

Ameipokea Abu Dawuud na At tirmidhy ????