BARUA YA HASSAN ALBASRI KWA ABDULLAZIZ AMIR ALMU’UMININ

Published on by شبكة منهاج السنة النبوية

Kasema Hassan Albasri kwa kuandika: Amma baad: Hakika Dunia ni nyumba ya unyonge na kupotea, na sio nyumba yenye kudumu,  kwa hakika ameteremshwa Adam hapa Duniani ni adhadu kwake, jihadhari nayo Ewe Amir Mu’uminin, kwa kuwa utakacho kikusanya utakiacha, na tajiri ndani yake ni masikini, inamdhalilisha atakaeitukuza, na inamtia umasikini mwenye kuikusanya, kama mfano wa sumu inamuagamiza isiomjua na yenyewe kuangamia, jihadhari na nyumba hii yenye kupumpaza yenye kudanganya, kuwa mwepesi kama utakuwepo ndani yake na jihadhari kama itakuwa kwako, furaha zake zimezungukwa na huzuni, na usafi wake umezungukwa na uchafu, laiti Muumbaji asingi tupa habari, na hakutupingia mifano juu yake, basi ilitosha kabisa kumuamsha alie lala, na kumtanabaisha alieghafilika, je vipi yamekuja makemeo makali kutoka kwa M.mungu, na ndani yake mawaidha,? Na alipewa Mtume wetu funguo na mali zake zote bila kupunjwa na chochote kwa M.mungu hata kama mfano wa ubawa wa Mbu akaikataa kuikubali, na kachukia kupenda alichokichukia Mola wake, au kukienzi alicho kidharau Muumbaji wake, kaiepusha M.mungu kwa Wachumungu kwa kutaka kwake, na kawafungulia maadui wake kwa kuwadanganya, je anadhani aliedanganywa nayo kwa kufunguliwa ya kwamba ndio kakirimiwa,? Na kasahau jinsi M.mungu alivyo mfanya Muhammad wakati akifunga Mawe tumboni mwake kwa njaa. Wallahi hakuna Mtu  yoyote yule aliefunguliwa Dunia na asiogope kuwa amedanganyika nayo, ispokuwa Mtu huyo awe amepungukiwa na akili na kuzorota mawazo yake.  

Abu Muadh Assalafii

+255773070222

To be informed of the latest articles, subscribe:
Comment on this post